Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Wachungaji Wawili wa KKKT Wafikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Mauaji.......Mmoja wa Moravian Mbaroni kwa Kukutwa na Meno 11 ya Tembo Kanisani

Wachungaji Wawili wa KKKT Wafikishwa Mahakamani Kwa Tuhuma za Mauaji.......Mmoja wa Moravian Mbaroni kwa Kukutwa na Meno 11 ya Tembo Kanisani

Picha
Wakati mchungaji wa Kanisa la Moravian akikamatwa na meno ya tembo 11 ndani ya kanisa, huko Moshi wachungaji wawili wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji. Tukio la wilayani Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro linawahusisha wachungaji wawili wa KKKT, Rodrick Mlay (52) na Godbess Mamkwe (38) pamoja na wananchi watatu ambao jana walipanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini humo kwa madai ya kuua kwa kukusudia. Wakati wachungaji hao wawili wakipanda kizimbani, Polisi mkoani Katavi kwa kushirikiana na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wanawashikilia watu wawili akiwamo mchungaji wa Kanisa la Moravian kwa tuhuma ya kunaswa wakiwa na meno ya tembo 11 wakiwa wameyahifadhi ndani ya kanisa. Akizungumzia meno hayo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alisema watuhumiwa hao walikamatwa juzi katika Kanisa la Moravian lililopo Kijiji cha Usevya, Wilaya ya Mlele. Nyanda alisema mchungaji huyo akiwa na mwenzake ...