Mkuu wa Mkoa Afumaniwa Akifanya Mapenzi na Mwanae
Mkuu wa zamani wa Mkoa wa Kaskazini Pemba na mshauri wa Rais wa Zanzibar kisiwani humo, Dadi Faki Dadi amekamatwa akituhumiwa kufanya mapenzi na mtoto wake wa kambo. Dadi alikamatwa juzi akidaiwa kukutwa na mtoto huyo wa mkewe wa ndoa mwenye umri wa miaka 21 katika nyumba ya kulala wageni inayoitwa Executive, jirani na makao makuu ya Uhamiaji Zanzibar katika eneo la Kilimani chini na Maisara, mjini Unguja. Mwanasiasa huyo alijikuta akipigwa pingu na polisi akiwa kifua wazi mbele ya mkewe na wanafamilia na kisha kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Mwembemadema. Picha za video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zilimwonyesha Dadi akikabiliwa na mashambulizi makali ya maneno kutoka kwa watu waliomkamata, akiwamo mkewe. “Mwacheni avae nguo kwanza, mpeleke bwana, twende bwana..." ni baadhi ya maneno yanayosikika katika video iliyorekodiwa wakati wa kumtia mbaroni. Taarifa zilizopatikana miongoni mwa wanafamilia ya kiongozi huyo, zilidai kwamba alikamatwa baada ...