Naibu Waziri Wa Mambo Ya Ndani Ya Nchi Afanya Ziara Gereza la Msalato – Dodoma
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema Serikali imejipanga kulitumia Jeshi la Magereza kuhakikisha Tanzania inaingia kwenye uchumi wa viwanda. Lengo hilo ni mkakati wa wizara kutaka kuendana na kauli ya Rais John Magufuli ambaye amekuwa akisisitiza kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda kuelekea kwenye uchumi wa kati ifikapo 2025. Masauni aliyasema hayo jana alipotembelea mradi wa kiwanda cha kokoto cha Gereza la Msalato kilichopo Dodoma. Alisema Magereza ina rasilimali nyingi ambazo zikitumika kikamilifu zinaweza kuifanya nchi kupiga hatua. Alisema kuna fursa nyingi ambazo jeshi hilo linaweza kuzitumia kufikia azma hiyo, ikiwamo kuanzisha kiwanda cha viatu kwa ajili ya askari wa majeshi mbalimbali. “Inashangaza kuona majeshi yetu yananunua viatu kutoka nje wakati vinaweza kutengenezwa na Magereza.Lazima tujipange na ninaamini Jeshi la Magereza linaweza kuifanya kazi hiyo,” alisema Masauni. Akizungumzia mradi wa kokoto wa gerez...