Serikali Yatoa Bilioni 2.3 Kuwalipa Wafanyakazi Wa NIDA
SERIKALI imeipatia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Shilingi Billioni 2.3 (Bilioni mbili na milioni mia tatu) kwa ajili ya kuwalipa waliokuwa watumishi wa muda wa mamlaka hiyo, wapatao 597, waliosimamishwa kazi hivi karibuni. Malipo hayo yanahusisha mishahara yao ya miezi minne, ukiwemo mshahara wa mwezi mmoja wa notisi ya kusimamishwa kazi, pamoja na malimbikizo ya madeni yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii. Kabla ya NIDA kuwalipa watumishi hao fedha hizo, Wizara ya Fedha na Mipango iliamua kufanya uhakiki ili kujiridhisha kama madai hayo yalikuwa sahihi. Uhakiki huo ulihusisha mahojiano ya ana kwa ana na watumishi hao pamoja na kupitia nyaraka mbalimbali zikiwemo majalada, mikataba ya ajira, madaftari ya mahudhurio, taarifa za kazi za kila siku na namba zao za akaunti za benki zilizokuwa zikitumika kulipa mishahara. Katika uhakiki huo imebainika kuwa kulikuwa na kasoro ama changamoto kadhaa zikiwemo za kimikataba kati ya NIDA na watumishi hao. Wakati wa zoezi hilo, ...