Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya 000

Video : Jionee wizi mpya wa mpesa na tigo pesa, jamaa kaibiwa 720,000

Picha
Utapeli umekua mwingi sana hapa mjini, watu wengi wanatapeliwa kila siku. Kutapeliwa ni kutapeliwa tu haijalishi ujanja utakaotumika ni wa sasa au wa zamani. Ila siku za karibuni kumetokea aina mpya ya utapeli ambao wahathirika wakubwa ni watu wanaotoa huduma za Mpesa na Tigo Pesa. Kama utakavyoona katika video hii ni ngumu sana kugundua kama umeshatapeliwa mpaka baada ya mdaya mda upite. Kwa mfano huyu jamaa aliyetapeliwa hapa kaibiwa 723,000 na matapeli hao. Hebu tazama video hii na wewe usije ukaibiwa kama huyu.

Serikali Yanasa Kilo 34,000,000 za Sukari Mafichoni

Picha
Shehena ya sukari ya kilo milioni 34 zilizokuwa zimefichwa kwenye maghala ya wafanyabiashara watatu Kilimanjaro imekamatwa na vyombo vya usalama, na serikali mkoani humo imetangaza kuiuza kwa wananchi kuanzia jana kwa bei elekezi ya Sh. 1,800. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecki Sadiki alithibitisha jana kukamatwa kwa shehena hiyo, baada ya makachero wanaoongoza timu maalumu ya ukaguzi wa maghala ya wafanyabiashara na mawakala wa sukari kubaini kufichwa kwa bidhaa hiyo. “Tumefanya ukaguzi katika maghala 45 na katika harakati hizo tumenasa tani 34 (kilo milioni 34) za sukari iliyokuwa imefichwa,"  alisema. "Katika zoezi hilo kuna mfanyabiashara mmoja mkubwa, yeye alikutwa na tani 31.33 lakini alikuwa akiiuza, isipokuwa bado tumewapa kazi Mamlaka ya Mapato (TRA) ichunguze kama imehodhiwa isivyo halali,”  alisema Sadiki. Kiasi cha sukari iliyobakia, alisema Mkuu wa M koa huyo, kilikamatwa kwa wafanyabiashara wengine wawili, ambao walikuwa na tani nne kasoro,...

Comoro: jina la rais mtarajiwa mikono mwa wapiga kura 6,000

Picha
Mwanamke huyo wa Comoro akiwa mbele ya orodha ya majina ya wagombea katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais Februari 22, 2015 Moroni. AFP/Aboubacar M'CHANGAMA Na  RFI Nchini Comoro, wapiga kura 6,300 wanatarajiwa kupiga kura leo Jumatano katika muendelezo wa uchaguzi wa urais ulioitishwa baada ya vurugu wakati wa duru ya pili ya uchaguzi. Kura ya uamuzi wa kuamua kati ya kiongozi wa zamani wa mapinduzi Azali Assoumani na mgombea wa utawala unaomaliza muda wake " Mamadou ". Kanali Assoumani, ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi hiyo kuanzia mwaka 1999 hadi 2006, alikua akiongoza katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais wa Aprili 10, kwa 40.98% ya kura, kwa mujibu wa matokeo ya awali. Lakini anamshinda mshindani wake Mohamed Ali Soilihi "Mamadou" kura 2,000 tu sawa na 39.87% ya kura. Duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Comoro ilikubwa na machafuko, hasa katika kisiwa cha Anjouan ambapo masanduku ya kura yaliharibiwa na watu kudhalilishwa katika vituo vya ku...

Nigeria ina wafanyakazi hewa 24,000

Picha
 Serikali ya Nigeria imeondoa karibu wafanyikazi 24,000 kutoka kwa orodha ya malipo ya wafanyikazi wa umma baada ya uchunguzi kugundua kwamba majina hayo yalikuwa ghushi. Wizara ya fedha imesema hatua hii imesaidia kuokoa kima cha dola bilioni 11.5. Hii ni moja wapo ya kampeni ya kupambana na ufisadi aliyo ahidi Rais Muhammadu Buhari alipochukua mamlaka mwaka uliopita. Ufisadi na usimamizi mbaya wa fedha za umma zimetajwa kama vizingiti vikubwa dhidi ya ukuaji wa Nigeria, ambapo serikali imelazimika kubana matumizi kutokana na tisho la mdororo wa uchumi. Nigeria ndiyo yenye uchumi mkubwa zaidi Barani Afrika na pia inaongoza katika uzalishaji wa mafuta imekumbwa na matatizo ya kifedha hususan kutokana na kuanguka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. Nchi hiyo pia inakumbwa na mfumuko wa bei, kuanguka kwa soko la hisa huku uchumi huo ukiwa na ukuaji wa chini zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya muongo mmoja.