Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Ni hatari

DIAMOND PLATINUMS ALI KIBA KIMENUKA TENA,NI HATARI, MAZITO YAFUMUKA

Picha
Stori: Mwandishi Wetu,  Kimenuka! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mafahari wawili wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kutupiana vijembe vya kufa mtu baada ya kuwepo kwa madai ya Kiba kuhujumiwa. Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’. Kwa mujibu wa chanzo makini, ili kuweka hujuma ya kibiashara, hivi karibuni, pamoja na kukanusha mara kadhaa kutokuwa na tatizo na Kiba, Diamond alidaiwa ‘kutengeneza’ kwa makusudi penzi la mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe na msanii wa Wasafi Classic Baby (WCB), Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’ kisha kuvujisha video ya uhusiano huo mpya siku ambayo Kiba alikuwa akiuachia wimbo wake mpya wa Aje (Jumamosi iliyopita), lengo likiwa kuhamisha upepo mashabiki kutoka kwenye wimbo mpya na kujali mapenzi ya wawili hao. Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. “Ni hujuma ya kibiashara, Diamond na uongozi wake wameamua kumfanyia Kiba ili wimbo wake...

Mbongo Anaswa na Unga wa Bil. 10,Ni hatari

Picha
Herry Mussa Yangealiyenaswa na ‘unga’. Stori:  Makongoro Oging’, UWAZI DAR ES SALAAM: Hii ni funga kazi sasa! Kuna habari kwamba, Mtanzania anayejulikana kwa jina la Herry Mussa Yange (42), amenaswa na polisi nchini Botswana akiwa na madawa ya kulevya ‘unga’ yenye thamani ya shilingi bilioni 10.5, Uwazi limefukunyua. Polisi wakikagua mzigo huo. ILIVYOKUWA Alikuwa akiusafirisha kwa lori (semitrela). Alitokea DRC na wenzake wawili. Avuka mipaka ya nchi kadhaa, akamatiwa Sauzi. Shehena ya unga aliyokamatwa nayo. Polisi wa Sauzi wamstukia, watumia mbinu za Kiintelijensia kumnasa. Akutwa na mifuko 141 ya Unga aina ya mandrax, paketi 1,000 ndani yake. Wafunguliwa mashtaka hukohuko. Uwazi lanena na Kamanda wa Polisi wa Kitengo cha Kupambana na Kuzuia Madawa ya Kulevya Tanzania, ACP Mihayo Msikhela, alikiri kupokea taarifa hizo. Kamanda wa Viwanja vya Ndege Tanzania, ACP Martin Otieno yeye anasemaje kuhusu Mtanzania huyo kama alipitia katika viwan...