NYAMA NYEKUNDU NA ZA KUSINDIKWA ZINASABABISHA SARATANI YA TUMBO
Taasisi ya Shirika la Afya Duniani (WHO) inayohusika na tafiti juu ya saratani, IARC (The International Agency for Research on Cancer) ilifanya tafiti juu ya hatari ya saratani ya utumbo kutokana na matumizi ya nyama nyekundu na ya kusindikwa. Kabla ya hapo, nyama nyekundu na za kusindika zimekuwa zikihusishwa na saratani ya utumbo pamoja na magonjwa ya moyo na shinikizo la damu. Maana Ya Nyama Nyekundu na Nyama Ya Kusindikwa Nyama nyekundu ni nyama inayotokana na misuli ya wanyama aina ya mamalia kama ng’ombe, mbuzi, kitimoto, kondoo, swala, nyati, punda, mbwa, panya na kadhalika. Nyama ya kusindika ni nyama iliyowekwa chumvi, kukaushwa, kuokwa kwa moshi au kemikali za kuisaidia kukaa muda mrefu bila kuharibika au kutopoteza ladha yake. Nyama ya kusindika inaweza kuwa ya ng’ombe, nguruwe, kuku, kondoo n.k. Baadhi ya nyama za kusindika ni kama hotdogs, ham, sausages, nyama za kopo n.k. Matokeo ya utafiti huu uliotangazwa tarehe 26 Oktoba 2015 yanaonesha kuwa utumiaji wa...