Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Walimu Dar tumieni fursa ya usafiri

Walimu Dar tumieni fursa ya usafiri

Picha
Hivi karibuni wamiliki wa vyombo vya usafiri kupitia umoja wao wa (DARCOBOA na UWADA) walifikia muafaka wa kutoa huduma ya usafiri bure kwa walimu wa shule za msingi na sekondari katika Mkoa wa Dar es salaam ikiwa ni hatua ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali katika kuinua sekta ya elimu. Hatua hii ilikuja baada ya kupokea ombi la Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mheshimiwa Paul Makonda, kuwaomba wamiliki hao kuangalia namna ya kuwapunguzia adha ya usafiri walimu ikiwa kama mchango wao katika sekta ya elimu. Hatua hii ilipokelewa na wadau wa elimu katika mitazamo tofauti huku asilimia kubwa wakilipokea kwa mtazamo chanya na kuona kwamba jamii inaanza kuona thamani ya mwalimu na mchango katika maendeleo ya taifa letu. Hata hivyo wapo baadhi ya watu ambao kwa makusudi wameamua kupotosha dhana hii na kujenga hofu miongoni mwa walimu kwamba upo uwezekano wa walimu kuzalilishwa na madereva na makondakta wa mabasi ya abiria. Kwa upande wetu madereva na makondakta, tukiwa kama wadau ...