Siku 67 za Ombeni Sefue Ikulu Kabla ya Kutumbuliwa JIPU Jana
JANA ilikuwa siku ambayo Rais John Magufuli alitoa uamuzi mzito wa kubadilisha nafasi za uongozi wa ngazi ya juu zaidi kwa viongozi ambao amefanya nao kazi baada ya kumuondoa Balozi Ombeni Sefue aliyekuwa katibu Mkuu Kiongozi, akiwa mstari wa mbele kutangaza wanaotumbuliwa majipu. Balozi Ombeni Sefue alikuwa kivutio cha wengi kwenye vyombo vyahabari kutokana na kutoa taarifa za kutenguliwa uteuzi kwa watumishi waandamizi wa umma, lakini jana hali ilikuwa tofauti baada ya kibao kugeuka. Ombeni Sefue aliibukia kuwa kipenzi cha vyombo vya habari katika muda mfupi aliofanya kazi na Rais Magufuli, huku mitaani akivuta wengi karibu na runinga kila alipoonekana, hasa kutokana na wananchi kutarajia kusikia habari za kutumbuliwa kwa majipu ambao umekuwa ukifanywa na Serikali tangu Rais aapishwe Novemba 5, 2015. Alianza kuchukuliwa na wengi kuwa ni mchapakazi na muadilifu na angeweza kwenda na kasi ya Rais Magufuli, ambaye amekuwa akihimiza mambo hayo na kusisitiza kuwa mtu ...