Ujumbe wa AU wakamilisha safari yake Burundi
Ujumbe wa AU wakamilisha safari yake Burundi Ujumbe wa Umoja wa Afrika uliokuwa umetumwa nchini Burundi kutafuta suluhisho la mgogoro wa nchi hiyo umekamilisha safari yake nchini humo baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Rais Pierre Nkurunziza.Mazungumzo ya ujumbe huo na Rais wa Burundi yaliendela kwa muda wa masaa manne japokuwa hadi sasa hakujatolewa taarifa yoyote kuhusu kilichojadiliwa kati ya pande hizo mbili.Afisa mawasiliano wa ikulu ya Rais wa Burundi, Willy Nyamitwe amesema mazungumzo hayo yamekuwa na matunda ya kuridhisha lakini kambi ya upinzani inasema haina matumaini na matokeo ya mazungumzo. Kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Afrika, Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amebakia nchini Burundi na anasema safari hiyo imekuwa na mafanikio.Baadhi ya ripoti zinasema serikali ya Bujumbura imekubali kuketi kwenye meza ya mazungumzo na kambi ya upinzani chini ya usimamizi wa jamii ya kimataifa.Ujumbe wa Umoja wa Afrika nchini Burundi ulijumuisha Marais Jacob Zuma wa Afrika Kusini...