Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Charles Kitwanga : Serikali Haifichi Mkataba wa Lugumi

Charles Kitwanga : Serikali Haifichi Mkataba wa Lugumi

Picha
Charles KitwangaWAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga amesema serikali haifichi mkataba wowote ukiwamo wa Lugumi Enterprises, isipokuwa wabunge wanapaswa kufuata taratibu ili kuona mikataba hiyo kama kanuni zinavyowaelekeza.  Kitwanga alisema hayo juzi usiku bungeni wakati akifanya majumuisho ya mjadala wa hotuba yake ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2016/17. Kuliibuka mjadala mzito kuhusu masuala ya mikataba ukiwamo wa Lugumi na Jeshi la Polisi, kiasi cha kuwa moja ya sababu za wabunge wa upinzani kukataa kusoma maoni yao kuhusu hotuba hiyo ya Waziri Kitwanga.  Kitwanga alipojibu hoja za wabunge, alisema hakuna anayeficha mikataba yoyote katika wizara hiyo kwani hata hiyo mikataba inayozungumzwa aliiwasilisha katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama alipotakiwa kufanya hivyo.  “Hata huu mkataba wa Lugumi unaweza kuonwa na mbunge yeyote ila kuna taratibu zake. Pia wabunge msisahau haya ni masuala ya usalama, yanaiweka nchi kat...