Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Makamu Mkuu wa Shule Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumlawiti Mwanafunzi Wake

Makamu Mkuu wa Shule Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumlawiti Mwanafunzi Wake

Picha
MAKAMU Mkuu wa Shule ya Sekondari Usevya katika Halmashauri ya Mpimbwe wilayani Mlele , Makonda Ng’oka “Membele” (34) amefikishwa katika Mahakama ya mkoa wa Katavi kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wake. Mshtakiwa huyo alifikishwa juzi mbele ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Chiganga Tengwa ambapo alikana shitaka lake na yupo nje baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kulipa kiasi cha Sh 3,000,000 mahakamani. Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Gregory Mhangwa alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo katika shule ya sekondari Usevya kati ya Novemba 2015 na Aprili 2016. Alieleza mahakamani hapo kwamba katika kipindi hicho mshtakiwa alimuingilia mwanafunzi wake huyo kinyume cha maumbile. Hakimu Tengwa aliahirisha shauri hilo hadi Juni 26 , mwaka huu litakapotajwa tena. Inadaiwa kuwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa Makamu Mkuu huyo wa shule hiyo kunafuatia wanafunzi wa kiume wanaosoma Kidato cha Tano katika shule hiyo kumkat...