Umri unakuzuiaje kuolewa na umpendaye?
Karibu tena msomaji wangu katika uwanja wetu huu maalum ambapo tunaelimishana kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi. Wiki iliyopita tulianza kujadili kuhusu mada ya madhara yanayosababishwa na mwanamke kumzidi umri mpenzi wake. Tuliishia kuangalia changamoto zinazojitokeza kwa wapenzi ambao wapo ndani ya aina hii ya uhusiano. Changamoto ya kwanza ilikuwa ni heshima na nyingine ni vikwazo kutoka kwa ndugu. Nakushukuru msomaji wangu ambaye umeshiriki kwa kutuma ujumbe mfupi na kueleza hisia zako kuhusu mada yetu. Leo tunaendelea na changamoto nyingine zinazowakabili watu ambao wapo kwenye aina hii ya uhusiano. WATOTO Kibaiolojia, mwanamke akishafikisha umri wa kuanzia miaka 40- 45, mzunguko wake wa hedhi hufikia mwisho au kwa kitaalam huitwa Menopause. Mwanamke akifika katika hatua hii, anakosa uwezo wa kuzalisha mayai na kutunga mimba. Kama mwanamke wa namna hii akioana na kijana mdogo ambaye bado damu inachemka na anahitaji kuwa na watoto, kikwazo kikubwa kita...