Umri unakuzuiaje kuolewa na umpendaye?

Karibu tena msomaji wangu katika uwanja wetu huu maalum ambapo tunaelimishana kuhusu masuala mbalimbali yahusuyo uhusiano wa kimapenzi.

Wiki iliyopita tulianza kujadili kuhusu mada ya madhara yanayosababishwa na mwanamke kumzidi umri mpenzi wake.

Tuliishia kuangalia changamoto zinazojitokeza kwa wapenzi ambao wapo ndani ya aina hii ya uhusiano. Changamoto ya kwanza ilikuwa ni heshima na nyingine ni vikwazo kutoka kwa ndugu. Nakushukuru msomaji wangu ambaye umeshiriki kwa kutuma ujumbe mfupi na kueleza hisia zako kuhusu mada yetu.

Leo tunaendelea na changamoto nyingine zinazowakabili watu ambao wapo kwenye aina hii ya uhusiano.

WATOTO
Kibaiolojia, mwanamke akishafikisha umri wa kuanzia miaka 40- 45, mzunguko wake wa hedhi hufikia mwisho au kwa kitaalam huitwa Menopause. Mwanamke akifika katika hatua hii, anakosa uwezo wa kuzalisha mayai na kutunga mimba.

Kama mwanamke wa namna hii akioana na kijana mdogo ambaye bado damu inachemka na anahitaji kuwa na watoto, kikwazo kikubwa kitakuwa ni ukweli kwamba mwanamke husika hataweza kumzalia mtoto. Je, ni wanaume wangapi wanaoweza kukubali kuwaoa wanawake wakati wakijua fika kwamba hawawezi kuwazalia watoto?

Kama mwenzi wako akiridhika mwenyewe, basi uhusiano wenu utaendelea kudumu bila hata kuwa na watoto.

KUCHANGANYA FAMILIA
Wanawake wengi, mpaka anafikia hatua ya kuwa mtu mzima, utakuta tayari alishawahi kuzaa na wanaume wengine. Kama bado umri haujafikia ukomo wa hedhi, akiolewa anaweza kuzaa watoto wengine lakini kazi inakuja katika kuchanganya familia.

Watu wengi hushindwa kuwa- treat kwa usawa watoto waliozaliwa ndani ya ndoa na wale wa nje hivyo kama nyote hampo makini, mtaishia kujenga matabaka kati ya wale waliozaliwa na mama kwa wanaume wengine na wale waliozaliwa kwenye ndoa.

Kama mmependana ni vyema kila mmoja kuwa muwazi kama alishawahi kuzaa watoto na kwa pamoja mkubaliane kwamba hakutakuwa na ubaguzi wa watoto.

Kama mkikubaliana kuhusu hili mapema, mtaishi kwenye uhusiano wenye amani lakini kama ikishindikana, itakuwa kinyume chake.

USUMBUFU WA WASICHANA WA RIKA LAKE
Kama wewe ni mwanamke na umependana na mwanaume ambaye kiumri ni mdogo kuliko wewe, kihaiba lazima atakuwa anatamani kuwa na uhusiano na wasichana wa rika lake. Wakati mwingine ni wasichana hao ndiyo watakaokuwa wanamsumbua mtu wako kwa kuwaona kuwa hamuendani na wao ndiyo ‘wanamechi’.

Ukiingia kwenye uhusiano wa namna hii, lazima uwe makini na ukubaliane kupambana na changamoto hii.

UMRI SI KIKWAZO KATIKA MAPENZI

Mwisho ningependa kumalizia kwamba umri si tatizo kabisa katika suala zima la mapenzi. Usikubali kelele za watu zikufanye umpoteze unayempenda eti kwa sababu ni mdogo kwako. Shughulikia changamoto zote nilizozielezea tangu wiki iliyopita na ukiwa na msimamo thabiti, utaishi naye vizuri licha ya tofauti iliyopo kati yenu.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA