SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 29 Machi 2016

T media news

MKWASA ALIA KUIKOSA CHAD



DAR ES SALAAM


KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars Charles Mkwasa amesema kitendo cha Chad kujitoa kwenye michuano ya Afrika kimemnyong’onyesha. Chad iliyokuwa icheze mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu kwa fainali za michuano ya Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) 2017 dhidi ya Stars jana, ilitangaza kujitoa kutokana na ukata.

Akizungumza , Mkwasa alisema timu yake ilishajiandaa kushinda mechi ya jana na kwamba wachezaji walikuwa kwenye ari kubwa. Katika mechi ya kwanza iliyochezwa mjini N’Djamena Jumatano iliyopita, Stars ilishinda bao 1-0 na kufufua matumaini kwenye michuano hiyo.

“Baada ya ushindi ule wachezaji wangu walikuwa kwenye ari kubwa na walikuwa na uhakika wa kushinda mechi ya marudiano, lakini jambo la kujitoa kwa wapinzani wetu limetunyong’onyesha wote,” alisema.

Aidha Mkwasa alilaumu kwamba vitendo kama jivyo ndivyo vinavyosababisha soka ya Afrika haipigi hatua kwa baadhi ya nchi kutokana na kutokuwa makini. “Soka ya Afrika kwa baadhi ya nchi haiwezi kwenda mbele zaidi, hili linakatisha sana tamaa hatuna tu la kufanya,” alisema.