SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 30 Machi 2016

T media news

Myanmar yamwapisha rais wake wa kwanza raia


Myanmar yamwapisha rais wake wa kwanza raia
Htin Kyaw ameapishwa rasmi kama rais wa kwanza kuchaguliwa kwa njia ya kidemokrasia, na hivyo kuhitimisha utawala wa kijeshi wa zaidi ya miongo mitano nchini humo.
Rais Htin Kyaw kutoka chama cha upinzani cha National League for Democracy (NLD) amekula kiapo cha utiifu bungeni hii leo katika mji mkuu Naypyidaw pamoja na makamu wake wawili.
Akila kiapo cha kuongoza nchi, Rais mpya wa Myanmar ameahidi kuwa atakuwa mtiifu kwa nchi na watu wa taifa hilo, na pia kuheshimu katiba na sheria za nchi. Chama cha upinzani cha NLD kinachoongozwa na mwanasiasa mkongwe Bi Aung San Suu Kyi mwezi Novemba mwaka jana kilishinda asilimia 80 ya viti vya uwakilishi bungeni. Hata hivyo Suu Kyi mwenyewe hakuweza kugombea kiti cha urais kwa sababu ya masharti yaliyomo ndani ya katiba ya Myanmar ambayo yanamuondoa katika nafasi ya kugombea mtu yoyote aliye na mke, mume au watoto wa nchi ajinabi. Watoto wawili wa Bi Suu Kyi ni Waingereza ambao alizaa na muwe wake aliyefariki dunia.