KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI AKIFUNGUA JIWE LA MSINGI LA KIWANDA KIPYA CHA VIFUNIKO WILAYANIN KIBAHA MKOA WA PWANI
NA Sosy
TANZANIA ya viwanda anayoitaka Rais John Magufuli imeenza kumea ambapo leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji Dkt Dkt. Adelhelm Meru amefungua jiwe la msingi katika kiwanda cha vifungashio kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Hiyo ni dalili njema na sio ya kubeza tayari tulichoahidi Rais Magufuli kinaanza kufaniwa kazi.
Wachambuzi wa Masuala ya uchumi nchini wametabiri kuwa Tanzania ikiwekeza kwenye viwanda uchumi utakuwa haraka ambapo itapelekea nchi kuwa tajiri yenye uchumi nzuri.
KATIBU MKUU WA WIZARA YA VIWANDA UWEKEZAJI NA BIASHARA AKIZUNGUMZA BAADA YA UFUNGUZI WA JIWE LA KIWANDA KIPYA
Leo katika uzinduzi huo Dkt Meru amesema kuwa mpango wa kukuza uchumi wa nchi unategemea viwanda hivyo wakuu wa mikio na wilaya wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano na wawekezaji pamoja na serikali kwa kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji.
Dkt Meru amesema kuwa viwanda vitaongeza pato la taifa kwa asilimia 15 na kuongeza kuwa ajira zitaongezeka kwa asilimia 40 hadi kufikia mwaka 2020.
Mtendaji mkuu wa shirika la Maendeleo la taifa (NDC) Mlingi Mkucha ameahidi kuwa shirika hilo litaendelea kutoa ushiirikiano kwa wawekezaji ili kufikia malengo ya serikali ya awamu ya tano ya kufikia katia uchumi wakati kupita viwanda.
Mkucha ameongeza kuwa wilaya ya kibaha inaeneo la hekari 330 za kuwekeza kwenye viwanda mbalimbali pamoja na viwanda vya kuunganisha magari, viwanda vya madawa ya binaadamu pamoja na nguo ambazo