SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 30 Machi 2016

T media news

Fat-h na Hamas zaafikiana kutekeleza maelewano ya kitaifa


Fat-h na Hamas zaafikiana kutekeleza maelewano ya kitaifa
Mwakilishi wa Harakati ya Fat-h huko Ghaza amesema kuwa hakuna makubaliano mapya katika ajenda ya kazi, bali kile kilichopo ni kufikiwa makubaliano kuhusu utekelezaji wa maelewano ya kitaifa ya Palestina.
Yahya Rabah ameashiria safari ijayo ya Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina mjini Doha Qatar kwa ajili ya mazungumzo na Khalid Mash'aal Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati yay Hamas ili kutekeleza muafaka wa mapatano ya kitaifa na kueleza kuwa, jumbe za harakati za Hamas na Fat-h zimefikia makubaliano kuhusu masuala yote ya kisiasa ya pande mbili na kwamba hakuna suala ambalo halijapatiwa ufumbuzi.
Yahya Rabah ameongeza kuwa ujumbe wa harakati ya Fat-h utarejea karibuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ili kuwataarifu viongozi wa harakati hiyo kuhusu mapatano hayo.
Mwakilishi wa Fat-h huko Ghaza amezungumzia pia mpango wa kisiasa wa serikali ya Palestina kwamba wameafikiana kuwa mpango wa kisiasa wa serikali uwe kama ule wa Harakati ya Ukombozi ya Palestina.
Awali Ziyad al Dhadha Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas aliashiria kumalizika mazungumzo kati ya Hamas na Fat-h huko Doha Qatar na kueleza kuwa mazungumzo hayo yamekuwa na natija chanya kuhusu namna ya kutekeleza mapatano ya kitaifa ya Palestina.