SIKU 7 ZA DKT SHEIN ZANZIBAR ZIMEKATIKA, ATAFUATA KAULI AU KATIBA?




Dkt. Shein aliapishwa kuwa Rais wa Zanzibar Alhamishi ya March 24, 2016 ambapo kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar inamtaka awe amemtangaza Makamu wa Kwanza wa Rais katika kipindi cha siku saba tangu kuapishwa. Ingawa mpaka sasa ameshampata makamu wa pili wa Rais visiwani humo.

Hali imekua Tofauti sana kwa Mshindi wa Uchaguzi Mkuu wa Marudio Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein,  kwakuwa aliahidi anataka kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa kutoka miongoni mwa vyama 13 vilivyoshiriki katika uchaguzi huo uliosusiwa na chama cha wananchi CUF, pamoja na vyama vingine Saba.

Dr Shein alitangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC,Jecha Salimu Jecha kuwa mshindi katika Uchaguzi huo kwa kupata asilimia 91.4 % ya Kura Zote zilizopigwa.

Chama kilichofuatia kwa matokeo hayo ni Alliance for Democratic Change ADC, ambacho Mgombea wake Hamad Rashid Mohamed, alipata asilimia 3.0% ya kura zote.

Kutokana na matokeo hayo, inaonesha kuwa hakuna chama cha Upinzani kilichofikisha aslimia 10% ya kura ambazo zingetosha kuunda SUK na CCM na Pia hakuna chama kilichopata walau kiti kimoja katika Baraza la Wawakilishi na Kushika nafasi ya pili kama Katiba ya Zanzibar Inavyotaka.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA