Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amesisitiza juu ya kuundwa nchi huru ya Palestina.
Mahmoud Abbas, ameashiria juhudi anazofanya kwa ajili ya kuundwa nchi huru ya Palestina na kueleza kwamba anakusudia kuitisha mkutano wa kimataifa utakaohudhuriwa na nchi zote duniani ili kuhitimisha suala la kuundwa nchi huru ya Palestina.
Pamoja na hayo, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina ameashiria kuendelea utawala wa Kizayuni wa Israel na sera zake za ujenzi wa vitongoji na kueleza kuwa sharti la kufanyika mkutano huo wa kuhatimisha kadhia ya Palestina ni kusimamishwa kwanza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni na kukamilishwa mwenendo wa amani na Israel.
Hii ni katika hali ambayo, katika kuendelea kutekeleza sera zake za kujipanua, utawala ghasibu wa Kizayuni umekusudia kujenga nyumba nyengine mpya 900 huko Baitul Muqaddas Mashariki.
Lengo la utawala haramu wa Israel la kupanua vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi unazozikalia kwa mabavu ni kubadilisha muundo wa idadi ya watu kwa manufaa ya wazayuni.