Johan Cruyff ni jina ambalo limeandikwa sana mwishoni mwa wiki kwenye tasnia ya michezo na sio kuandikwa tu bali watu wengi walivyoguswa na msiba huo wa mtu aliyefanikiwa katika zama zake za kucheza na kufundisha mpira wa miguu.
Pamoja na vilabu vya Ajax na Barcelona alivyovichezea na kufundisha kwa mafanikio makubwa kuomboleza kwa aina yake, Chama cha soka nchini uholanzi kinalo jambo mhimu kinafikiria kufanya kwaajili ya gwiji huyo aliyeiletea heshima nchi na sasa wanapanga kubadili jina la uwanja wa Amsterdam Arena na huenda ukapewa jina la JOHAN CRUYFF.
Michael van Praag, rais wa FA uholanzi alisema: “Siwezi kusubiri kwa muda wakati ndio huu kwa sisi kubadili jina la uwanja wetu na kuwa Johan Cruyff Arena Na hii ndio njia bora tunaweza kumlipa..”
Amsterdam Arena kwasasa ni dimba la nyumbani kwa Ajax na timu ya taifa ya Uholanzi na ulifunguliwa rasmi mwaka 1996. Cruyff alishinda mataji nane na makombe matatu ya Ulaya wakati akiichezea Amsterdam kabla ya kutimkia Barcelona.
Baada ya kuhama Barcelona mwaka 1973 Cruyff alichezea Los Angeles Aztecs, Washington Wanadiplomasia na Levante, kabla ya kurejea Ajax na hatimaye kustaafu akiwa na Feyernoord. Cruyff pia alipata mafanikio makubwa akiwa kocha wa Barcelona kwa kushinda mataji manne ya La Liga na Kombe la Ulaya.