Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haifuati siasa za madola ya Magharibi hususan Marekani.
Ayatullah Sadeq Amoli Larijani amesisitiza kuwa, Iran haitekekelezi siasa na mambo yao kwa mujibu wa matakwa ya Marekani
Mkuu wa Vyombo vya Mahakama vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria uvunjaji ahadi wa Marekani na kubainisha kwamba, kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Marekani inalionesha taifa la Iran makali ya pande mbili za mkasi na hivyo kulitaka taifa hili lisisalimu amri mbele yake au likabiliwe na vikwazo.
Ayatullah Amoli Larijani ameashiria suala la "uchumi wa kimuqawama" na kusema kwamba, wananchi wa Iran katu hawataacha kuyatetea malengo yao ya Mapinduzi ya Kiislamu hata kama watakabiliwa na vikwazo zaidi vya kiuchumi na mashikizo zaidi ya Marekani.
Mkuu wa Vyombo vya Mahakama nchini Iran ameeleza kuwa, njia ya wananchi wa Iran ni izza na mamlaka ya kujitawala na ili kufikia malengo hayo kuna udharura wa kufanikiwa uchumi wa kimuqawama kwa kutegemea uzalishaji wa ndani.