SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 29 Machi 2016

T media news

Wapinzani Nger: Tupo tayari kuzungumza na Rais Issoufou


Wapinzani Nger: Tupo tayari kuzungumza na Rais Issoufou
Wapinzani nchini Niger wametangaza azma yao kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais Mahamadou Issoufou wa nchi hiyo.
Chama kikuu cha upinzani ambacho pia kimetangaza kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita nchini humo, kimeyasema hayo baada ya kukutana na Brigi Rafini, Waziri Mkuu wa nchi hiyo. Katika taarifa yake, chama hicho kinachoongozwa na Hama Amadou, kimetangaza utayarifu wake kwa ajili ya kuzungumza na rais huyo aliyeibuka mshindi katika uchaguzi huo. Aidha chama hicho kimetaka mazungumzo hayo yawe ya kweli na jadi kwa ajili ya kumaliza mgogoro wa kisiasa ambao unaendelea nchini Niger tangu kujiri uchaguzi mkuu uliopita. Rais Mahamadou Issoufou aliibuka mshindi baada ya kupata asilimia 94/92 ya kura katika uchaguzi wa duru ya pili uliofanyika tarehe 20 mwezi Machi mwaka huu. Chama kikuu hicho cha upinzani kiliutaja uchaguzi huo kuwa wa kimaonyesho suala ambalo lilisababisha chama hicho kuususia.