SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 29 Machi 2016

T media news

Mapigano ya kikabila Côte d’Ivoire watu kadhaa wauawa


Mapigano ya kikabila Côte d’Ivoire watu kadhaa wauawa
Kiongozi mmoja wa eneo la mpakani kati ya Côte d’Ivoire na Burkina Faso ametangaza kutokea mapigano makali ya kikabila kaskazini mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa afisa huyo, mapigano makali ya kikabila yamejiri katika mji wa Bouna, kaskazini mashariki mwa Côte d’Ivoire na karibu na mapaka wa Burkina Faso. Afisa huyo wa serikali amesema kuwa, katika mapigano hayo watu wasiopungua 22 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa. Amesema kuwa, chanzo cha mapigano hayo kati ya wakulima na wafugaji, ni kufuatia wafugaji kugombania ardhi. Aidha maapigano hayo chanzo chake kikuu kinatajwa kuwa ni wimbi la wakimbizi kutoka nchi mbili hizo. Itafahamika kuwa, maelfu ya raia wa Côte d’Ivoire wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto, waliyakimbia makazi yao kufuatia kuibuka mapigano ya kikaumu na hivyo kuamua kuelekea nchini Burkina Faso. Jumapili iliyopita mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Aïchatou Mindaoudou alizitaka pande hasimu kujizuia na kumaliza uhasama baina yao. Aidha Mindaoudou alitaka kupelekwa askari wa kofia ya buluu katika eneo hilo kwa minajili ya kumaliza mgogoro huo.