Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Mkuu wa Wilaya Amzuia Waziri Nchemba Kwenda Kijijini Kusikiliza Kero za Wananchi

Mkuu wa Wilaya Amzuia Waziri Nchemba Kwenda Kijijini Kusikiliza Kero za Wananchi

Picha
Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Annarose Nyamubi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mara, juzi alimzuia Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mwigulu Nchemba kwenda kijiji cha Mikomario wilayani Bunda kutatua mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji kwa madai ya wasiwasi wa usalama kuwa mdogo.  Baada ya jitihada zake za kumzuia kugonga mwamba, Nyamubi ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Bunda aliamua kujitenga na ziara hiyo kwani licha ya kufika eneo la mkutano, hakujihusisha na lolote kwa kuamua kukaa pembeni.  “Mheshimiwa waziri nakushauri usiende Kijiji cha Mikomario kwa muda huu ambao unakaribia usiku kwa sababu usalama utakuwa ni mdogo kutokana na ukorofi wa wananchi wa eneo lile,” alishauri Nyamubi wakati akizungumza na Nchemba ofisini kwake. Hata hivyo, waziri Nchemba alisisitiza kuwa lazima aende kuzungumza na wananchi hata kama atalazimika kuhutubia kwa kutumia taa za gari kwa sababu aliwaahidi kuwa angefika na kuzungumza nao na walikuwa wakimsubiri t...