Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya CCM Bunda Waanza Kumsaka Mchawi Aliyefanya Steven Wasira Kushindwa Uchaguzi

CCM Bunda Waanza Kumsaka Mchawi Aliyefanya Steven Wasira Kushindwa Uchaguzi

Picha
Jimbo hilo lilichukuliwa na Esther Bulaya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hivyo kumgalagaza mwanasiasa huyo mkongwe, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM.  Wapiga kura watatu walifunga kesi Mahakama Kuu kupinga ushindi wa Bulaya lakini hata hivyo walishindwa kuthibitisha udanganyifu wowote.  Kutokana na kushindwa huko kwenye sanduku la kura, wanachama wa CCM ‘wanakabana koo’ kwa tuhuma za kukisaliti chama hicho wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, na miongoni mwa wanaotajwa ni baadhi ya viongozi wake.  Taarifa zilizolifikia gazeti hili zinaeleza kuwa kamati ya siasa ya CCM katika kata ya Nyasura na viongozi wa matawi yake wanakamilisha taratibu za kuwavua uanachama vigogo wanne wa wilaya. Mbali na vigogo hao, CCM pia inataraji kuwafukuza wanachama wanne maarufu.  Katibu Mwenezi wa CCM katika kata hiyo, Frank Mamba alisema wanachama hao wameitwa kuhudhuria kikao kitakachowajadi...