Makamu Wa Rais Mhe. Samia Akutana Na Uongozi Wa Baraza La Tawla Na Uongozi Wa Skaut Leo
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kazi kubwa ya Chama Cha Skauti wa Kike nchini hivi sasa ni kuhakikisha kinarejesha heshima ya mwanamke katika jamii. Samia ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akizungumza na baadhi ya wanachama wa chama hicho waliofika ofisi kwake Ikulu kwa ajili ya kuelezea shughuli zao katika kusaidia watoto wa kike waweze kujitambua na hatimaye kulitumikia Taifa. Alisema pamoja na chama hicho kinafundisha kujenga ujasiri na kuwa huru kwa mtoto wa kike lakini kuna haja ya kukumbushana umuhimu wa kuzingatia mila na desturi nzuri zilizopo katika matendo yao ili kurejesha heshima ya mwanamke. "Sasa hivi utakuta binti kavaa kipanti kinambana hasa, anazunguka barabarani huku na kule, mwenyewe anajiona yuko sawa...hicho ni kinyume kabisa na maadili yetu, mila na desturi zetu za kiafrika tumeziacha kabisa." alisema Makamu wa Rais. Aidha alisema katika enzi hizi za utandawazi kumekuwa na urushwaji wa mambo yasiyo na maadili katika mitandao jambo ambalo m...