Moïse Katumbi kusikilizwa kwa mara nyingine na Mwendesha mashitaka
Moise Katumbi aimarisha timu yake ya wanashria wa Congo kwa kumshirikisha mwanasheria kutoka Ufaransa Eric Dupond-Moretti. www.katanga.cd Na RFI Moïse Katumbi anatazamiwa kusikilizwa tena leo Jumatano na Mwendesha mashtaka mjini Lubumbashi katika mfumo wa uchunguzi kuhusu madai ya kuajiri askari mamluki wa kigeni. Baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya saa saba Jumatatu wiki hii, Moïse Katumbi ameamua kuimarisha utetezi wake, kwa kumshirikisha katika timu yake ya wanasheria wa Congo mwanasheria mashuhuri wa chama cha mawakili nchini Ufaransa: Wakili Eric Dupond-Moretti. Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga na mgombea urais anatuhumiwa na mahakama ya nchi hiyo " kuajiri askari mamluki" , hasa Wamarekani. Mwanasheria wa masuala ya jinai kutoka Ufaransa, Eric Dupont-Moretti, amekubali kumtetea mpinzani wa DR Congo Moise Katumbi, Mei 10, 2016. © AFP/MEHDI FEDOUACH "Mashirika ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu yanasema kuwa kesi hii haieleweki, na kesi ya kisiasa ...