Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Rais wa zamani wa Sudan ataka Waislamu waungane dhidi ya Israel

Rais wa zamani wa Sudan ataka Waislamu waungane dhidi ya Israel

Rais wa zamani wa Sudan, Abdurahman Suwar al-Dhahab ametoa wito wa kuweko mshikamano baina ya Waislamu ili kuweza kuzima njama za utawala haramu wa Israel dhidi yao.Al-Dhahab amekumbusha kauli ya rais wa kwanza wa utawala haramu wa Israel, David Ben-Gurion ambaye aliwahi kusema kuwa wazayuni wanafaa kufanya juu chini kuhakikisha Waarabu watapigana wenyewe kwa wenyewe na kusahau maslahi yao ya pamoja na kusisitiza kuwa sasa matamshi hayo yanashuhudiwa kivitendo. Rais wa zamani wa Sudan ametoa wito huo wa umoja pambizoni mwa mkutano wa maulamaa wa Kiislamu mjini Jakarta huko Indonesia. Abdurahman Suwar amesema matatizo mengi yanayoukumba ulimwengu wa Kiislamu yanatokana na kufeli Waislamu kuungana na kuhifadhi malengo yao ya pamoja. Amesema kutokana na ukweli huo, adui mzayuni amepata mwanya wa kuzidisha ukiritimba, dhulma na manyanyaso dhidi ya Wapalestina.