Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Upande wa Pili wa Mkasa wa Ndoa ya Tiwa Savage Utakuacha Mdomo Wazi

Upande wa Pili wa Mkasa wa Ndoa ya Tiwa Savage Utakuacha Mdomo Wazi

Picha
Mume wa Tiwa Savage, Tee Billz alipost mfululizo wa malalamiko kwenye Instagram kuhusu kumtuhumu mke wake kuwa alimsaliti na Doj Jazzy, Dr Sid na 2Face Idibia.  Jamaa huyo alionesha nia ya kutaka kujiua kutokana na masahibu hayo. Hiyo ilipelekea jamii kubwa ya Nigeria imchukie Tiwa kwa kumuona kama mwanamke katili na anayemtesa mumewe. Lakini upande wa pili wa shilingi wa mkasa huo unaweza ukabadili mawazo yako.  Kwa mujibu wa Tiwa, mume wake ndiye mzinguaji mkubwa na ana vimbwanga haswaa.  Akiongea kwenye exclusive interview na Pulse TV, Tiwa alisimulia jinsi ambavyo mume wake alikuwa akimfanyia ikiwa pamoja na kumtelekeza kwa kutotaka kujua chochote pale alipolazwa hospitali nchini Jamaica alikoenda kufanya video na Busy Signal.  Anasema wakati anajiandaa kwenda kushoot, alianza kutoka damu nyingi ukeni kiasi cha kupoteza fahamu. Alimpigia simu na kumtumia ujumbe mumewe ikiwa pamoja na kumtumia picha akiwa hoi kitandani lakini hakujibiwa hadi anatoka hospital...