Nimechoka kudanganya kila siku - Mo Music
Msanii Mo Music ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa 'Skendo' amefunguka na kusema kuwa kwa sasa amechoka kusema uongo na kuwadanganya mashabiki zake juu ya kazi zake na ukimya wake kwenye muziki. Mo Music akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na ting'a namba moja kwa vijana alidai kuwa mara nyingi amekuwa akitoa ahadi zisizo timia kwa mashabiki wake kutokana na menejimenti yake kushindwa kazi yake, ikiwepo kumfanyia video pamoja na jambo ambalo limekuwa likimkwamisha na kumrudisha nyuma. "Unajua uongozi wangu umefika sehemu ambayo kwa sasa kwangu kuvumilia imekuwa ni ngumu kwa sababu mwanzo walinichukua kama ndugu na tuliishi kama ndugu, kwa sasa nimefanya nao kazi huu mwaka wa tatu mimi napiga jalamba lakini sioni mafanikio yoyote kiuchumi, na mimi saizi ni majukumu mengi kuna watu wanasoma kwa ajili yangu mwenyewe natakiwa kuendesha maisha kwa kazi hivyo kazi zinapokuwa haziendi nazidi kukwama mimi" alisema Mo Music. Mbali na hilo ...