Zitto ‘Amchana Laivu’ Rais Magufuli..Adai Bado Hafanyi Inavyopaswa.......
ZITTO Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT- Wazalendo amesema, Rais John Magufuli anapapasa suala la ufisadi, anaandika Pendo Omary. Amesema, serikali yake bado haijachukua hatua madhubuti katika vita dhidi ya rushwa nchini licha ya ‘shangwe’ nyingi. Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya ACT- Wazalendo. “Bado Rais hafanyi inavyopaswa, bado rais anapapasa suala la ufisadi. Kuna mambo ya muda mrefu ambayo tunaendelea kama nchi kuyalipua lakini arais ameyakalia kimya. Mfano ni suala la Tegeta Escrow,” amesema Zitto na kuongeza; “Bado mtambo wa IPTL upo chini ya matapeli na kila mwezi serikali inawalipa matapeli hawa zaidi ya Sh. 8 bilioni wazalishe au wasizalishe umeme. “Hivi ndio vikundi maslahi katika sekta ya nishati ambavyo bila kuvibomoa, rais ataonekana anachagua katika vita hii.” Zitto amesema, serikali imeficha inaowaita madalali wa rushwa katik...