Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya WANACHAMA WA YANGA WACHOMA MOTO MAGAZETI YA REGINALD MENGI ..KISA MANJI

WANACHAMA WA YANGA WACHOMA MOTO MAGAZETI YA REGINALD MENGI ..KISA MANJI

Picha
Wanachama wa Yanga wamecharuka na kufanya kitendo kinachoonyesha ni hasira kutokana na kuchana na kuchoma moto magazeti. Wanachama hao wa Yanga, leo wamechoma moto magazeti ya Nipashena The Guardian katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Jangwani na Twiga, Kariakoo jijini Dar es Salaam. Wanachama hao wamefanya hivyo wakipinga Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kusakamwa kw amakusudi na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi. “Hii sasa imetosha, huyu Mengi na magazeti yake anamsakama Manji kila anapoona Yanga inafanya vizuri. Mara tu baada ya Yanga kutinga robo fainali hatua ya Kombe la Shirikisho, basi vyombo vyake vimeanza kuandika kwamba anatakiwa sijui kuondolewa Coco Beach. “Hakuna asiyejua Manji amestaafu Quality Group, sasa anamtaja wa nini. Au anataka ashindwe kufanya kazi za Yanga kwa utulivu. “Watuache, kweli tutatangaza watu wa Yanga waachane na kununua bidhaa zake,” alisema Abuu Chehekah...