Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Waziri Makamba Awasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

Waziri Makamba Awasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.

Picha
Serikali inaendelea kusimamia mazingira na kuhakikisha mifuko ya plastiki inayotumika nchini iwe ni ile inayokidhi viwango vianavyokubalika ili kuondokana na changamoto ya kuzagaa kwa mifuko hiyo katika maeneo mbalimbali.  Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba alipokuwa akitoa hoja ya wizara yake kuidhinishiwa maombi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2016/2017.  Makamba amesema kuwa sababu kubwa ya kusambaa kwa mifuko ya plastiki inatokana na mifuko hiyo kutolewa bure na hivyo kuchafua mandhari na kuziba mifereji sehemu mbalimbali hali inayosababisha athari kubwa katika mazingira.  “Asilimia kubwa kwenye mito, maziwa na fukwe za bahari imejaa mifuko ya plastiki, hali hii ni hari kwa usalama wa mazingira yetu” alisema Makamba.  Akiwasilisha hotuba yake, Waziri Makamba amesisitiza kuwa mifuko ya plastiki isiyotakiwa kutumika nchini ni ile yenye unene chini ya maikroni ...