Chadema Waungana na CUF Kutomtambua Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetangaza rasmi kutoitambua Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), inayoongozwa na Dk Ali Mohamed Shein. Mbali na kutoitambua Serikali hiyo, chama hicho kimesema leo kitatoa mkakati mzito wa namna ya kushughulikia suala la matangazo ya Bunge la Kumi na Moja kutoonyeshwa moja kwa moja (live) na televisheni. Msimamo huo ulitangazwa kwa waandishi wa habari jana mjini Dodoma katika kikao cha pamoja kati ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji, manaibu wake wawili, John Mnyika (Bara) na Salum Mwalimu (Zanzibar). Pia walitoa taarifa juu ya mambo yanayojadiliwa katika kikao cha siku mbili cha Kamati Kuu (CC) kinachofanyika chini ya Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe. Akizungumzia hali ya kisiasa Zanzibar, Mwalimu alisema chama hicho hakitampa ushirikiano Dk Shein. “Kikao maalumu cha Kamati Kuu ya Chadema kilichoketi Jumatatu, tumefikia msimamo wa kutoitambua Serikali ya SMZ. Msimamo wa Maalim Seif Sharif...