Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Hali nchini Syria baada ya kuanza utekelezwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano

Hali nchini Syria baada ya kuanza utekelezwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano

Picha
Tangu kuanza utekelezwaji wa makubaliano ya usitishaji vita kati ya serikali na wapinzani huko Syria Ijumaa iliyopita, mambo mengi yamejitokeza ambayo yanatujengea taswira ya jinsi hali halisi ilivyo katika nchi hiyo na eneo zima la Mashariki ya Kati.Kuanza mchakato wa kujiandikisha watu kwa ajili ya kuwania viti vya ubunge kwenye uchaguzi ujao, kuendelea vyema utekelezwaji wa makubaliano hayo ambayo hayayahusishi makundi ya kigaidi kama vile Daesh na Jab'hat an-Nusra, kufukuzwa makumi ya raia wa Syria kutoka Kuwait, radiamali ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria kwa matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia Adel al-Jubeiri, pamoja na mashambulizi ya wapiganaji wa Kikurdi dhidi ya ngome za Daesh ni baadhi tu ya matukio hayo ya Syria tangu kupotea kwa kiasi kikubwa sauti za risasi na mizinga katika nchi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.Tume ya uchaguzi ya Syria imetangaza kuwa, kufikia jana Jumatatu takriban watu 3000 walikuwa wamejiandikisha kama wagombea wa viti vya ubunge...