Chadema yachambua siku 120 za Magufuli
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimezichambua siku 120 za Rais John Magufuli tangu ashike wadhifa huo kikidai kuwa uongozi wake umetawaliwa na ukiukwaji wa haki, demokrasia na utawala bora. Aidha, Kamati Kuu ya chama hicho iliyokutana hivi karibuni imeitisha mkutano wa Baraza Kuu utakaofanyika Machi 13 jijini Mwanza ambao utatoa msimamo wa jinsi chama hicho kikuu cha upinzani kitakavyoidai haki badala ya kuiomba na kuweka mkakati wake kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020. Kasoro zilizotajwa kushikia hatamu katika siku hizo zilizotimia jana ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuendesha uchaguzi kwa upendeleo na haki kutotendeka Zanzibar baada ya kufutwa kwa uchaguzi, kuingiliwa kwa uchaguzi wa wenyeviti wa halmashauri na mameya, kuthibiti Bunge na uundwaji wa kamati na viongozi wake, polisi kuzuia mikutano ya hadhara na wabunge na madiwani wa Chadema kukamatwa kwa sababu zisizo za msingi. Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maazimio ya kikao hicho, Mwenyekiti wa Chadema, ...