Azam yamaliza kazi wa Bidvest
Kocha msaidizi wa Azam, Mario Marinica amesema wameshaipeleleza vya kutosha klabu ya Bidvest WitsWachezaji wa Azam wakisikiliza ushauri wa kocha wao wa Mario Marinica wakati wa mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mbeya iliyofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi. Picha na MaktabaDar es Salaam. Kocha msaidizi wa Azam, Mario Marinica amesema wameshaipeleleza vya kutosha klabu ya Bidvest Wits watakayokutana nayo Jumamosi na kuahidi kuwa watapata ushindi.Azam itapambana na Bidvest Jumamosi nchini Afrika Kusini katika mchezo wa raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) utakaoanza saa 12:00 jioni.Marinica aliyekwenda Afrika Kusini kuitazama Bidvest ikiilaza Lightstars ya Shelisheli kwa mabao 6-0 katika mchezo wa nyubani ilishinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-0.Katika safari hiyo, kocha huyo aliongozana na mwenzake, Dennis Kitambi aliyesema kazi imekamilika. Kocha huyo, raia wa Romania alisema wanatakiwa kumaliza tatizo la kushindwa kutumia vyema nafasi...