Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Utata Wazuka Kuhusu Mtu Aliyepoteza Maisha Kwenye Ajali ya Tundaman

Utata Wazuka Kuhusu Mtu Aliyepoteza Maisha Kwenye Ajali ya Tundaman

Picha
Utata umeibuka kuhusu mtu aliyefariki kwenye ajali ya gari aliyokuwa amepanda Tundaman kutokea Njombe kuja Dar es Salaam, Jumapili hii.  Kwenye ajali hiyo, alifariki dereva aliyekuwa akiendesha aliyejulikana kwa jina la Man Katuzo. Hata hivyo imebainika kuwa, Katuzo hakuwa tu dereva, bali ndiye alikuwa bosi wa Tunda kwenye show hiyo na ndiye aliyekuwa akigharamika kwa kila kitu. Taarifa hiyo imebainika kupitia segment ya ‘Simu ya Mwisho’ inayoendeshwa na rapper Baghdad kupitia kipindi cha Papaso cha TBC FM.  Hii ni taarifa ambayo Baghdad ametutumia baada ya kuongea na ndugu wa marehemu:  Baghdad alizungumza na kaka wa marehemu ambaye ndiye msemaji wa familia juu ya kifo cha mdogo wake ambapo alithibitisha taaarifa ya kifo cha mtu mmoja ambaye hamkumtaja jina ambaye alikuwa ameketi siti ya mbele na kusema kweli Tundaman alikuwepo kwenye gari iliyopata ajali lakini hakuumia.  Aidha kaka yake aliendelea kusema ya kuwa amesikitishwa na kitendo cha wakat...