Kabla ya ndoa jiulize, kwa nini umempenda
Mahusiano Uamuzi wa ndoa si wa kujaribu. Unatakiwa kujihakikishia kwamba ni kweli umevutiwa na kila kitu cha mwenzako, kwamba utakuwa naye katika shida na raha. Hayo ndiyo mambo ya kuzingatia. Nimeshaandika mengi kuhusu sifa za anayetakiwa kuoa au kuolewa, lakini nasogea mbele zaidi na kuangalia sababu za kumpenda mtarajiwa wako katika ndoa.Zipo sababu za msingi sana ambazo unatakiwa kuwa nazo kabla ya kuingia kwenye ndoa KWA NINI UJIULIZE Lazima nifafanue hili kwanza kabla ya kuendelea. Hivi unafikiri ni kwa nini ni lazima kujiuliza sababu za kumpenda mwenzi wako? Yes! Ni kwa lengo la kujiwekea usalama katika ndoa yako ijayo. Kujiandalia amani na pumziko la kweli. Kwenye mapenzi ya dhati pekee ndipo vinapopatikana vitu nilivyotaja hapo juu. Kwa maneno mengine kuwa na majibu ya swali linalosomeka kwenye kichwa cha mada hii ni kujihakikishia ndoa bora. Tuendelee kujifunza. NI MWENZI WA NDOTO ZAKO? Jambo kubwa kuliko yote ambalo unatakiwa kuliangalia kwa jicho la tatu ni kama mw...