Kujiunga Sudan Kusini na Jumuiya ya Afrika Mashariki
ukubwa wa hati Kichapishi Add new commentSudan Kusini imejiunga na Jumuiya ya Kieneo ya Afrika Mashariki (EAC).Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania ambaye ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Mashariki alitangaza habari ya kupatiwa uanachama Sudan Kusini katika Jumuiya ya EAC katika kikao cha jana cha viongozi wa nchi za jumuiya hiyo. Kikao cha Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kilifanyika katika mji wa Arusha kaskazini mwa Tanzania.Shirika la habari la Ufaransa limeripoti kutoka Dar es Salaam Tanzania kwamba baada ya kujiunga Sudan Kusini, nchi wanachama wa EAC zimefikia sita ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini. Nchi hizo zina jamii ya watu karibu milioni 150.Jumuiya hiyo ya kieneo inajishughulisha na kuzihamasisha nchi wanachama kushirikiana katika masuala ya biashara na kurahisisha suala la ushuru wa mpakani kati ya nchi wanachama.Sudan Kusini mwezi Julai mwaka 2011 ilijitenga na Sudan na kujitangaza kuwa huru baada y...