Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) Sasa Kuendeshwa Kijeshi

Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) Sasa Kuendeshwa Kijeshi

Picha
WIZARA ya Maliasili na Utalii imeridhia maombi ya Shirika la Hifadhi la Taifa (TANAPA) kubadili mfumo wa utendaji kazi kutoka ule wa kiraia na kuwa jeshi usu (Paramilitary) ili kukabiliana na tatizo sugu la ujangili wa wanyamapori, misitu, na rasilimali nyingine za nchi. Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya askari na wahifadhi wa shirika hilo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Gaudence Milanzi alisema maombi ya shirika hilo kutaka kubadilishwa na kuendeshwa kwa sheria za kijeshi ni ya msingi katika kipindi hiki ambacho Tanzania inakabiliwa na tatizo sugu la ujangili wa wanyamapori. Ufungaji wa mafunzo hayo ulifanyika juzi katika kambi ya Mlele ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi mkoani Katavi ambako askari 101 na wahifadhi 26 walihitimu mafunzo ya kijeshi ya miezi mitatu hadi sita  “Kwa sasa uhifadhi unakabiliwa na changamoto kubwa ya ujangili,hususan tembo na faru kuporomoka kwa maadili ya askari na uingizaji wa mifugo hifadhini,”  alisema Meja Jene...