Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya MASAUNI AONGOZA VIONGOZI WA SERIKALI KUHANI MSIBA WALIOCHINJWA KITONGOJI CHA KIBATINI MKOANI TANGA

MASAUNI AONGOZA VIONGOZI WA SERIKALI KUHANI MSIBA WALIOCHINJWA KITONGOJI CHA KIBATINI MKOANI TANGA

Picha
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimpa pole Hussein Mkola ambaye ni mtoto wa marehemu Mkola Hussein ambaye alichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi mwanzoni mwa wiki hii katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia nane zilizofiwa katika kitongoji hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo wakati alipokuwa anawasili msibani katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, mkoani Tanga, ambapo watu wanane walichinjwa na watu wanaohofiwa kuwa majambazi. Masauni alifanya ziara katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya wauaji hao, na baadaye alienda kutoa pole katika familia hizo zilizofiwa katika kitongoji hicho...