Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya VYAKULA VINAVYODHIBITI UZITO KUPITA KIASI

VYAKULA VINAVYODHIBITI UZITO KUPITA KIASI

Picha
Uzito kupita kiasi ni jambo la hatari kiafya kwa kila mtu, lakini zaidi kwa watu wenye umri mkubwa, wagonjwa na wale wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi (VVU). Watu wenye uzito kupita kiasi wako katika hatari ya kupata magonjwa mbalimbali yakiwemo shinikizo kubwa la damu, magonjwa ya moyo, kiharusi, kisukari cha ukubwani, miguu kuuma au kuvunjika mifupa. Uzito kupita kiasi pia, unaweza kuchangia kupunguza hamu na nguvu za kufanya tendo la ndoa kwa wadau wote wawili, hivyo ndoa inaweza kuwa katika wakati mgumu. Mara nyingi uzito kupita kiasi unasababishwa na mtu kukosa kufanya mazoezi au kazi za kutoka jasho, kuvuta sigara, kunywa pombe kwa wingi na ulaji usiofaa. Ulaji usiofaa ni pamoja na kula kwa wingi vyakula vya wanga, sukari na vile vyenye mafuta.  Kula kiasi kidogo vyakula vyenye nyuzi lishe kama vile mboga za majani na matunda ni muhimu. Zaidi walio katika hatari ya kupata uzito kupita kiasi ni wale wale wanaotumia vyombo vya usafiri kwa muda mwingi, wanaokaa ofisini au duk...