Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya ABANWA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU MWANAE

BABA YAKE DIAMOND PLATINUMS APATA KIBARUA,ABANWA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU MWANAE

Picha
 Inashangaza! Wakati wengi wanaamini mzazi hakosei, kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hali ni ya tofauti kwani licha ya kuaminika ana ukwasi wa kutosha, analalamikiwa kutomsaidia baba yake waliyetofautiana, Abdul Juma kiasi cha kukutwa akifanya kibarua cha kumenya viazi vya chipsi ili apate senti za kujikimu, Risasi Jumamosi limeinyaka. TUJIUNGE NA CHANZO Aprili 27, mwaka huu, Risasi Jumamosi likiwa katika harakati za kukusanya matukio, lilipigiwa simu na chanzo kilichoomba hifadhi ya jina ambapo kilivujisha habari kwamba, baba Diamond anafanya kibarua cha kumenya viazi katika eneo maarufu la kuuza chipsi lililopo Mtaa wa Liwiti- Kariakoo jijini Dar. SIKIA UBUYU HUU Chanzo: Hapo ni Risasi Jumamosi? Naongea na mhariri? Au nimekosea namba? Risasi Jumamosi: Hujakosea, hapa ni Risasi Jumamosi, karibu sana, kuna mpya? Chanzo: Yeah! Hivi mnajua kwamba baba Diamond anafanya kibarua cha kumenya viazi hapa Liwiti? Kuna  banda maarufu sana kwa chipsi. ...