Vigogo Chadema Kyela Wavuliwa Uongozi kwa Usaliti
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, Saadati Mwambungu pamoja na wajumbe 19 wa kamati ya utendaji wa wilaya hiyo, wamevuliwa uongozi baada ya kutuhumiwa kukihujumu chama. Hatua hiyo ilifikiwa juzi jioni na uongozi wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, chini ya mwenyekiti wake, Dk Stephen Kimondo na Mratibu wa Kanda, Frank Mwaisumbe na kuweka wilaya hiyo chini ya uangalizi wa uongozi wa Mkoa wa Mbeya ndani ya siku 30 wakati wakiendelea na uchunguzi. Mratibu wa Chadema katika Kanda hiyo, Frank Mwaisumbe alisema jana kuwa baada ya kufanyia kazi tuhuma 17 zilizowasilishwa kwao na wanachama wa chama hicho wilaya, walibaini kuwa tuhuma saba kati yake zina ukweli dhidi ya viongozi hao hivyo wakafikia uamuzi wa kuwasimamisha na kuwataka kurudisha mali zote za chama hicho ndani ya siku 30. “Ni kweli jana (juzi) tulifika Kyela na katika kikao chetu na kamati ya utendaji ya wilaya tulipowahoji ilionekana tuhuma saba zina ukweli na baadhi ya watuhumiwa walikiri. Miongoni mwa ...