Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Fuvu la Binadamu Ndani ya Ofisi ya Mwanamuziki Diamond Platnumz...

Fuvu la Binadamu Ndani ya Ofisi ya Mwanamuziki Diamond Platnumz...

Picha
Fuvu la binadamu lakutwa limewekwa kwenye meza ya Diamond pembeni ya picha ya mwanawe Tifah.  Diamond asema ni kweli ni fuvu la binadamu, ila ni pambo tu kama mapambo mengine, yeye anamtegemea Mungu.  Wakati mwenyewe akikanusha vikali kwamba hatumii ndumba kwenye muziki wake ambao sasa umemfikisha mbali kimataifa, staa wa Afro-Pop, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’, ameshikwa uchawi kufuatia kukutwa laivu kwa fuvu la binadamu ndani ya ofisi zake.  Fuvu hilo liko mkono wa kushoto mezani kwa Diamond huku jirani yake kukiwa na picha ya mwanaye, Latiffah Nasibu ‘Princess Tiffah’ iliyokuwa kwenye fremu.  Shuhuda mmoja aliyehudhuria hafla ya kusaini mkataba wa dili jipya alilosaini Diamond la Ubalozi wa Tomato Sauce ofisini kwake hapo alilithibitishia kuwepo kwa fuvu hilo lilozua gumzo kwa mashuhuda wachache wa tukio hilo.  “Ni kweli kuna fuvu la binadamu mezani kwa Mond (Diamond) but (lakini) sikufanikiwa kulishika kwa mikono ...