Mwalimu Atiwa Mbaroni Kwa Tuhuma za Kumkuwadia Mwanafunzi Wake
Mwalimu wa Shule ya Msingi Nyaigabo iliyopo Kijiji cha Musati wilayani Serengeti, Mkoa wa Mara anatuhumiwa kumkuwadia kijana anayemuuzia duka kwa kumpelekea mwanafunzi na kusababisha apate ujauzito. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhani Ng’hazi alisema mwalimu huyo, Agness Matiko amekamatwa na kuhojiwa kwa tuhuma hizo. Ng’hanzi alisema binti huyo mwenye umri wa miaka 16 alimaliza darasa la saba mwaka jana kwenye shule anayofundisha mwalimu huyo. Alisema mwalimu huyo alikuwa akimtoa darasani mwanafunzi na kumpeleka nyumbani kwake na kumkutanisha na kijana wake huyo kwa ajili ya kufanya naye ngono. Binti huyo alikuwa anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Ikorongo kabla ya kufukuzwa baada ya kubainika kuwa na mimba ya miezi sita. “Mwaka jana nikiwa darasa la saba mwalimu alinipeleka nyumbani kwake ili nikamsaidie kukamua ng’ombe maziwa, siku ya pili wakati wa mapumziko alinichukua nikamuoshee vyombo tulimkuta huyo kijana baadaye mwalimu alin...