Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Atoa Ushauri Wa Kupunguza Foleni Dar es Salaam

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Atoa Ushauri Wa Kupunguza Foleni Dar es Salaam

Picha
Rais mstaafu Jakaya Kikwete, amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kutekeleza mipango iliyowekwa na serikali yake endapo atahitaji kumaliza na msongamano katika jiji hilo. Kikwete alitoa ushauri huo jana, alipotembelea Daraja la Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam, huku akionyesha kuridhishwa nalo na kumtaka Makonda kuweka historia kama mkuu wa mkoa kijana kumaliza msongamano.    Alisema kuna mipango ambayo iliwekwa na serikali ya awamu ya nne katika kumaliza msongamano huo, ikiwamo uboreshaji wa reli ili kubabiliana na tatizo la usafiri, uboreshaji wa stendi za mabasi ya kwenda mikoani za Boko, Pugu na Mbezi Luis, ambavyo alisema ni muda mrefu sasa haoni utekelezaji wake.    “Kwa mfano kuna ile stendi ya Boko na mingine ni mipango ambayo iliwekwa lakini naona imekaa muda mrefu hakuna utekelezaji wake. Naona tu unakwenda unarudi, unakwenda unarudi, ”  alisema.    Kikwete alisema hakuna uchawi utakaosaidia kuma...