Je ni Kweli Supu ya Pweza Inaongeza Nguvu za Kiume? Ukweli Huu Hapa
HAMU ya tendo la ndoa kwa mwanadamu au mwanamke ni moja ya hisia za msingi kwa mtu wa kawaida kama ilivyo njaa au usingizi. Kwa ajili ya matatizo mbalimbali yaliyo katika jumuiya, pamoja na kwamba tendo la ndoa ni jambo la msingi kwa wale waliooana, kuna wanaume aidha hawana uwezo wa kulifanya tendo hili au wana hisia ndogo na nguvu kidogo za kutekeleza tendo hili. Panapokuwa na changamoto Fulani, wajasiriamali huiona changamoto hiyo kama fursa, na fursa hiyo imeonekana kuwanufaisha vijana wanaokaanga samaki aina ya pweza katika soko la samaki la kimataifa la magogoni baada ya supu ya samaki huyo aina ya pweza kuonekana kupendelewa sana na wanaume wa rika zote nchini. Lakini siku za hivi karibuni hiki kitumbua kimonekana kuingia mchanga, yaani biashara kuharibika baada ya uvumi kwenye mitandao ya kijamii kudai kwamba wakaanga samaki wanaweka dawa za kuongeza nguvu za kiume aina ya viangra ili kuisisimua miili ya wateja wao, Ni imani ya wanaume wengi wa pwan...